Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jussie Smollett atupwa jela

Jussie Smollett.jpeg Jussie Smollett

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji wa Marekani, Jussie Smollettt amehukumiwa kifungo cha siku 150 jela baada ya jopo la mahakama kugundua kuwa alidanganya polisi kuwa ameshambuliwa.

Nyota huyo wa zamani wa tamthilia ya Empire, mwenye umri wa miaka 39, alipatikana na hatia mwezi Desemba kwa mashtaka matano ya kufanya fujo baada ya kutoa taarifa za uongo kuhusu shambulio hilo la uwongo.

Adhabu hiyo pia inajumuisha miezi 30 ambapo atakaa chini ya uangalizi na kutozwa faini ya dola 145,000 (£110,000) sawa na Tsh 335,766,491. Kesi hiyo ilitokana na tukio la miaka mitatu iliyopita ambapo Smollett alisema alishambuliwa na watu wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live