Mwanqmuziki mkongwe, Juma Kassim ‘Sir Nature’juzi ameachia ngoma yake aliyoipa jina la Assalam Alaykum ikiwa ni mahususi kwa ajili ya mwezi wa mfungo wa Ramadhani.
Nature amezungumza hayo nasi akifafanua kuwa ameamua kufanya hivyo ili kusindikiza kipindi hiki kwa ujumbe maalumu na muhimu kwa jamii nzima katika kutakiana heri na kusalimiana kwa unadhifu.
“Unajua hiki ni kipindi muhimu kwetu wote na nitaachia wimbo wa Asalaam Aleykum ukiwa maalumu kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani tulionao sasa, tusalimiane kwa hekima na ni salamu yenye heri, hivyo le watapokea ujumbe muhimu,” amesema Nature.
Aidha, pia ameeleza kuwa kwa sasa anasubiri kumalizika kwa Ramadhani ili aachie rasmi EP (Extended Playlist) ambayo itakuwa na mchanganyiko wa ladha za muziki wake zenye vionjo tofauti safari hii.
“Lakini pia watu wasubirie ujio wangu baada ya kumalizika kwa mwezi, ninakuja na EP yangu niliyoipa jina la Sauti Moja, kama kawaida itakuwa na ladha tofauti na vionjo vya juu maana kama unavyofahamu mimi huwa nasikilizwa na wengi na hupenda kumgusa kila mmoja,” amesema Nature.