Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juma Nature agoma kufanya shoo Wasafi Festival

Naturesss 2 Juma Nature agoma kufanya shoo Wasafi Festival

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Kassim Ally maarufu kama Juma Nature amegoma hakutumbuiza kwenye Tamasha la Wasafi Festival mjini Mtwara Wikiendi iliyopita.

Mkali huyo kutoka Kundi la TMK Wanaume ameshindwa kujing'ata ulimi ama kupindisha maneo na ameamua kuweka wazi kwanini aligomea shoo hiyp.

Hii ni baada ya shabiki kuuliza kwanini hakumuona wakati alitangazwa kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza ambapo mazungumzo yao kwenye Uwanja wa comments yalikuwa hivi.

Shabiki: Kirobotoo Jana mbona sijakudele wasafi na walikutangaza? Juma Nature: Nafanyaje show kwa laki tano mzee sidharau hizo.

Ni wazi kuwa huenda Wasafi walipanga kumlipa Tsh 500,000 hii ikamfanya Nature asusie kutumbuiza shoo hiyo kwa kuona ni kiwango kidogo kulinganisha na hadhi yake na uthamani wake kwenye historia ya kiwanda cha Bongo Fleva.

Wasafi Festival ilizinduliwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na baada ya hapo itasogea mpaka Dimba la Kassim Majaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live