Katika mitandao ya kijamii jana, Juni 3 zilienea taarifa kwamba gari lililokua limewabeba wasanii Juma Nature, Whozu, Stamina, Nandy, Barnaba, Roma, Billnass, Ice Boy na Willy Paul likielekea mkoani Sumbawanga, lilipata ajali katika eneo la Mikumi, mkoani Morogoro.
Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Juma Nature amesema ajali iliyotokea kwenye msafara wa Nandy Festival ulihusisha gari lililobeba vyombo vya muziki na baadhi ya wacheza shoo ambao hata hivyo hawakupata majeraha makubwa.
Akizungumza na MCL Didital leo Juni 4, Nature ambaye pia hufahamika kama Kibra amesema ajali ikitokea kila mtu huwa anaongea neno lake, ila ukweli ni kwamba wasanii wote wapo salama gari lililobeba vyombo vya muziki na baadhi ya wacheza shoo na wapiga vyombo ndilo lililopata ajali.
“Unajua kila mtu anaongea la kwake, ukweli gari la wasanii halikupata ajali ila lililopata ni gari lililobeba vyombo ambalo tulikuwa nalo katika msafara wa Nandy Festival.”
Naye, Nandy katika ukurasa wake wa Instagram ametuma kipande cha video kinachoelezea kuwa waliopata ajali ni waliokuwa kwenye gari lililobeba viongozi, wapiga vyombo vya muziki na wacheza shoo, na kwamba baadhi ya majeruhi wamesafirishwa kwenda Dar es Salaam.
Pia Soma
- Mwongozo kwa wanaoomba mikopo kujiunga Chuo Kikuu
- Uturuki yakomalia dili la makombora ya Urusi
- MAUAJI YA MWANAFUNZI WA SCOLASTICA :Tafrani yaibuka hukumu mauaji ya mwanafunzi wa Scolastica
- Makonda abaini upigaji vitambulisho vya machinga Kariakoo