Vita imezidi kupamba moto kati ya Mwanamama Zari kutoka Afrika Kusini na Mlimbwende Fantana (25) kutoka nchini Ghana, ambapo wawili hao wameitikisa mitandao ya kijamii ya Afrika baada kugombana vibaya huku chanzo kikiwa ni Mwanamuziki Staa,Diamond Platnumz.
Kwa mujibu wa Zari ambaye ndiye aliyeanzisha ugomvi na kuuleta mitandaoni ni kwamba Diamond akiwa chemba na Fantana alisema maneno ya uongo kwamba Zari bado anampenda Diamond na yupo tayari kumzalia mtoto wa tatu muda wowote endapo tu Diamond atataka kumrudia, jambo ambalo Zari alilikanusha na kusema Diamond aliongea uongo ili apate nafasi ya kupewa penzi ama kukubaliwa na Fantana.
Zari aliongeza kuwa yeye ni mwanamke mzuri, Bilionea asiyetegemea mwanaume, hata hivyo baadae Fantana aliibuka na kumcharaza vibaya Zari kwa ujumbe wenye maneno makari yenye ukakasi akipingana na majigambo ya Zari.
Kupitia kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM, Juma Lokole ambaye pia ni msemaji wa Diamond Platnumz amesema yeye amevutiwa sana Fantana na anastahili kuwa na Diamond kwasababu wanaendana, Lokole amemtaka Zari atulie kwani tayari walishaachana haina haja ya kuoneana wivu.
Aidha Juma Lokole amesema Zari bado anampenda sana Diamond ndiyo maana anaona wivu na kumchukia kila mwanamke anayekuwa na Diamond kiasi cha kuwaita wanawake wa Diamond (Makahaba).