Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julia Fox: Kuwa kwenye mahusiano na Kanye ni kama kulea mtoto

Julia Fox: Kuwa Kwenye Mahusiano Na Kanye Ni Kama Kulea Mtoto Julia Fox: Kuwa kwenye mahusiano na Kanye ni kama kulea mtoto

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji na mwanamitindo kutoka nchini Marekani Julia Fox amefunguka kuhusu mahusiano yake ya mwezi mmoja na Kanye West akidai kuwa yalikuwa kama analea watoto wawili kwa wakati mmoja.

Fox kupitia mahojiano yake na The Drew Barrymore Show ameeleza kuwa alishindwa kudumu kwenye mahusino hayo kwa sababu Kanye alikuwa anahitaji muda zaidi jambo ambalo mwanadada huyo alishindwa, kwani kwa wakati huo alikuwa na mtoto mdogo hivyo asingeweza kumuacha bila kumuhudumia.

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa alishangazwa na hakutarajia jinsi mahusiano yao yalivyo fahamika kwa kasi mitandaoni. Kanye West Fox walikuwa kwenye mahusiano mwaka 2022 lakini kwa sasa Kanye yupo kwenye mahusiano na mwanamitindo aitwaye Bianca Censori.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live