Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate aachia picha zake akiwa mjamzito

Jokate New Jokate aachia picha zake akiwa mjamzito

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya kwanza tangu ilipofahamika kwamba ni mama kijacho, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, DC Jokate Mwengelo ameachia picha zake za ujauzito na kuwapagawisha wengi wakiwemo mastaa kedekede nchini Tanzania.

DC Jokate ambaye wengine humuita Jojo au Kidoti ameachia picha hizo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuandika;

“Hakutakuwa na mwanamke yeyote atakayepoteza mimba wala kuwa tasa katika nchi yenu. Nami nitawajalia maisha marefu. ‭‭Kutoka‬ ‭23‬:‭26‬‭‬‬‬‬‬ “No one shall suffer miscarriage or be barren in your land; I will fulfill the number of your days. Exodus 23:26. AMEN…”

Kabla ya kuteuliwa na utawala uliopita wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na baadaye kuhamishiwa Wilaya ya Temeke katika utawala wa Awamu ya Sita, Jokate alikuwa staa wa urembo na mitindo, muziki na filamu, utangazaji na mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live