Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joh Makini: Kulipia youtube ni ukandamizwaji

A6c3ea8ee73557e0f742cf5e5be52dbd Joh Makini: Kulipia youtube ni ukandamizwaji

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya John Simon ‘Joh Makini’ amesema kulipia mtandao wa Youtube ulikuwa ni ukandamizaji wa vipaji na kuwakosesha ajira vijana.

Akizungumza Dar es Salam juzi alisema malipo hayo yalikuwa yakifanya wasanii washindwe kufikia malengo yao, hasa wale ambao wana kipato cha chini lakini wakiamini wana vipaji.

“Wasanii wachanga ambao hawawezi kwenda studio au kufanya kazi kubwa zaidi wamekuwa wakitumia mtandao wa Youtube kuonesha uwezo wao na watu wanawaona,” alisema.

Alisema kazi hiyo hailipi kama watu ambavyo wamekuwa wakifikiria, hivyo kuondoa tozo ni sawa na kusaidia mamilioni ya Watanzania waweze kujiajiri.

Joh Makini alisema lakini pia mitandao hiyo, itasaidia kuondoa vijana wasiokuwa na ajira na kusaidia kwa asilimia kubwa kuwafanya wajiajiri na kutotegemea ajira kutoka serikalini.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Hassan Abbasi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kukubaliana kutoa malipo kwa maudhui ya kazi za wasanii katika mtandao wa Youtube ambayo hayana mchakato wa habari.

Chanzo: www.habarileo.co.tz