Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joeboy: Grammy sio tuzo zetu

Joeboy 1200x675.jpeg Joeboy

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Afrobeats kutoka Nigeria, Joeboy amewakosoa wasanii wa muziki ambao wamekuwa wakisapoti shows za tuzo za nje na kusahau tuzo za ndani ya Afrika na kuwakumbusha kuwa tuzo za Grammy ni tuzo za Marekani hivyo wasikubali kila mwaliko wa tuzo hizo wahudhurie na kusahau tuzo zao za ndani.

Hitmaker huyo wa single kama Vibration amefunguka hayo kupitia Podcast ya The Big Convo nchini Ghana;

"Nadhani tunapaswa kuwa sisi na kuziwezesha tuzo zetu hapa Afrika, Grammy ni tuzo kubwa lakini bado ni tuzo ya Marekani, inachukuliwa kuwa tuzo ya kimataifa kwa sababu ya nafasi yake lakini sisi tunaifanya ionekane tuzo kubwa zaidi ambayo msanii wa Kiafrika anaweza kupata” – Joeboy.

Joeboy ameshauri wasanii wa Afrika kuzipa thamani tuzo za Afrika hata kama hazitakuwa na ukubwa wa Grammy kwa kipindi hiki, lakini ni muhimu kuziandaa na kuzifanya kwa level ya tofauti kuanzia uwekezaji, maandalizi ya shows na thamani ya tuzo zenyewe.

Una maoni gani pia kuhusu Tuzo za Muziki hapa nchini?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live