Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Jinsi ya kupika halfcake kwa ajili ya biashara

Half Cakes Recipe Main Photo Jinsi ya kupika halfcake kwa ajili ya biashara

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wengi wetu tunachukulia kupika halfcake ni jambo gumu lakini leo nimekuja kuvunja kauli hiyo kwa kuwaonesha na kuelekezana jinsi ya kutengeneza kitafunwa hicho ambacho wengi wetu hupendelea kukila kwa juice ama chai.

MAHITAJI

Unga nusu

Maziwa/maji

Yai 1

Sukari vijiko 6 vya kulia

Baking powder vijiko 2

Zafaran (yellow food coliring)

Vanilla powder kijiko 1 au vanilla ya maji (arki)

Hiliki 1/2 kijiko

Mafuta kwa ajili ya kukaangia

Chumvi kidogo

Siagi kijiko kimoja.

JINSI YA KUPIKA

Changanya viungo vikavu vyote (unga,sukari,chumvi,hiliki, baking powder)

Vunja yai alafu weka katika mchanganyiko wako ...weka siagi changanya vizuri

Weka maziwa kisha changanya vizuri hadi utengeze donge moja

Kanda hadi iwe laini lakini usiwe laini kama ule wa chapati huu unatakiwa uwe mgumu kidogo kisha subiri kwa dakika 30

Katakata halfcakes kutokana na shape unayopenda.

Weka karai jikoni kisha acha mafuta yapate moto kidogo na kaanga hadi ziive

ukitaka halfcake zako ziweze kupasuka vizuri inabidi usikaange kama unavyokaanga maandazi hapana cake hizi ukiweka zikaiva basi inabidi ushushe mafuta yapoe ndiyo uweke mkupuo wa pili mpaka utakapo maliza.

Kingine cha kuongezea mwendo ni ule ule lazima ufanye majaribio mara kwa mara kama unahitaji kwa ajili ya biashara hautakiwi kukurupuka siku unajifunza ndiyo siku unayotaka kuwauzia watu, ndugu yangu usifanye hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live