Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi wakili wa Wema Sepetu alivyojenga hoja mahakamani

65534 Wakili+pic

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Albert Msando, wakili wa mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amehoji sababu za shahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili mteja wake kutofika mahakamani, huku zikitolewa sababu zisizokuwa na ushahidi.

Msando ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 4, 2019 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu iliyomuachia huru Wema ambaye baadaye alikamatwa tena na askari wa Jeshi la Magereza.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.

Hakimu Mkazi Mkuu, Maira kasonde  alimwachia huru mshtakiwa huyo chini ya kifungu cha 225 (5) cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa Serikali,  Gloria Mwenda kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili kusikilizwa lakini shahidi waliokuwa wakimtegemea wamepewa taarifa kuwa anaumwa.

Baada ya maelezo hayo Msando amedai taarifa iliyotolewa mahakamani hapo haijajitosheleza, kuhoji kama mhusika alianza kuumwa jana au juzi, ilitakiwa kutolewa taarifa zinazojitosheleza.

Pia Soma

"Pande zote mbili zinatakiwa kutoa taarifa zinazojitosheleza. Nakumbuka mahakama ilitoa agizo kama ikitoke mtu anaumwa anatakiwa apeleke hati inayothibitisha.”

“Hilo ndio lilisababisha Wema kuwekwa rumande kwa wiki moja iweje huyo shahidi asifanye kama mahakama inavyotaka," amedai Msando akidai kwa zaidi ya siku 60 shauri hilo limekuwa likiahirishwa.

Kutokana na hali hiyo,  Msando ameiomba mahakama hiyo kutopokea ombi la upande wa mashtaka la kuahirisha shauri hilo.

Hata hivyo, Hakimu Kasonde amesema mahakama ilikuwa tayari kusikiliza kwa ushahidi tangu Machi28, 2019 lakini ilishindikana kutokana na upande wa mashtaka kutokuwa na mashahidi.

Kasonde amesema Aprili 18, 2019 pia ilitakiwa isikilizwe lakini upande wa mashtaka hawakuleta mashahidi hadi leo, kwamba  upande wa mashtaka wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo shahidi waliomuandaa ana udhuru au mgonjwa.

"Maofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ndiyo waliobaini tukio hili na hawa wapo hapa jijini Dar es Salaam ndio walioto taarifa polisi kwa nini wasije TCRA wa karibu mnataka mashahidi kutoka Arusha ," amehoji Masonde

Kasonde alisema kesi inapoamriwa kwa wakati inamfanya  mshtakiwa afanye maendeleo yake ya kiuchumi ili aweze kupata kipato na taifa kwa ujumla

Kutokana na hoja hizo, Hakimu alimuachia Wema huru chini ya kifungu cha 225(5) cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.

Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam alirekodi video ya ngono na kuisambaza katika ukurasa wa  mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

 

Imeandikwa na Pamela Chilongola, Daniel Francis na Sifras Kingamkono

Chanzo: mwananchi.co.tz