Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jimmy Kindoki amvaa Dulla Makabila "Ole wako"

Makabia Jimmy Kindoki amvaa Dulla Makabila "Ole wako"

Sat, 17 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Shabiki na Mwanachama wa Klabu ya Yanga Jimmy Kindoki amempa onyo msanii wa singeli Dulla Makabila ambaye ametangaza kuihama timu hiyo na kuhamia Simba kwa kusema hataki kumuona tena akirudi kwani amefanya kitendo cha usaliti kama Yuda.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumamosi , 17th Apr , 2021 Kushoto ni Jimmy Kindoki, kulia ni msanii Dulla Makabile

"Ole wako tusikie umerudi Yanga ndio utajua siku hiyo kama Yanga inawenyewe, mmekosa kiki kwenye muziki wenu sasa mnahamia huku, nikwambie tu hiyo furaha ya Simba ni ya muda mfupi siku huyo Moo akisema basi ujue Simba inarudi kwenye msoto"

"Halafu tukusike unaleta kiherehere chako baki huko huko uliposema unahamia huku hatuhitaji wasanii wasiojielewa na kwa kiongozi yoyote atakaemkaribisha huyu Yuda kwenye hafla za Yanga hatutaelewana" ameeleza Jimmy Kindoki

Siku chache zilizopita msanii Dulla Makabila aliweka taarifa ya kuihama timu yake ya Yanga kutokana na matokeo mabovu wanayoyapata kwenye baadhi ya michezo yao ya siku za hivi karibuni.

Chanzo: eatv.tv