Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jide: Msinipigie Mkiwa Mmelewa

Jide 660x400.jpeg Jide

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lady Jaydee au Jide; ni msanii mkongwe nchini Tanzania ambaye amewaonya watu ambao wana tabia ya kumpigia simu usiku hasa wakati wamelewa.

Kwa mujibu wa Jide, watu hao hufanya hayo ili kijionesha wako karibu naye, ilihali hawamuungi mkono kwenye kazi zake.

Kupitia Twitter, Jide ameandika; “Watu mnaonifahamu msiwe mnanipigia simu usiku mkiwa mmeshalewa baada ya kusikia nyimbo zangu huko mlipo ili watu waone mna ukaribu na mimi wakati you don’t even support my businesses wala shows hamji. Kuweni outsiders tu siwa-appreciate wala nini…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live