Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jibu la Jux kuhusu ujio wa albamu ya pamoja na Vanessa Mdee

1289 Vanessa Mdee TZW

Mon, 15 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Jux amefunguka iwapo kuna mpango wa kuja na albamu ya pamoja kati yake na Vanessa Mdee ambaye pia ni mpenzi wake.

Muimbaji huyo ameiambia Clouds Fm Top 20 bado hawajawa na mpango huo ingawa kila siku wanarekodi ngoma.

“Bado hatajupanga hilo lakini tunarekodi nyimbo, mara nyingi sisi wasanii tunakuwa tupo pamoja, tunatembea pamoja, pengine kama tutakaa sawa na menejimenti ya Vanessa na team yangu kwa sababu nje ya mahusiano yetu ni kazi pia,” amesema Jux.

“Kwa hiyo tunaweza tukasema tunaweza tukatoa albamu ya pamoja lakini siyo vitu ambavyo vipo tayari, ni mipango ambayo inaweza kuja baadaye,” amesisitiza.

Jux na Vanessa wameshatoa ngoma moja ya pamoja inayokwenda kwa jina la Juu, pia walishirikishwa na Nikki wa Pili katika wimbo ‘Safari’ ambao uliwakutanisha wasanii wengine kama Joh Makini, G Nako na Navy Kenzo.

Chanzo: bongo5.com