Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jibu la Damian Soul kwanini anafanya ngoma nyingi na Weusi (+video)

Video Archive
Tue, 20 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Muimbaji Damian Soul amefunguka sababu ya kufanya kazi nyingi na wasanii kutoka kundi la Weusi.



Akizungumza na Bongo5 Damian Soul amesema Weusi ni kama familia kwake na wamekuwa wakishauriana katika vitu vya kikazi ingawa ameshafanya kazi na wasanii kama Vanessa Mdee na Banana Zorro.

“We spend so much time together, imekuwa ni rahisi kufanya kazi mmnapokuwa pamoja, so mnajuana ni jinsi gani mnavyofanya kazi,” amesema.

“Mbali na hayo hawa wamenitangulia na wana fan base kubwa sana kwa hiyo ni kama support kwa brand yangu, unapofanya na Nikki ana mashabiki wake, G Nako, Joh Makini pia wana mashabiki wao, so unapokusanya wale mashabiki wanapata kunijua na Damian Soul anazidi kukua kila siku,” amesisitiza.

Damian Soul amefanya ngoma mbili na Joh Makini ambazo ni Penzi na Baraka, amefanya ngoma moja na G Nako iitwayo Tudumishe, pia amefanya ngoma moja na Nikki wa Pili inayokwenda kwa jina la Data.

Chanzo: bongo5.com