Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jibu la Banky W kwa wanaomkosoa kupinga kufanya harusi za mbwembwe

1827 Bankyw Wedding

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Staa wa muziki kutoka Nigeria Banky W ameamua kufunguka na kueleza kile anachokiamini baada ya wengi kukosoa uamuzi wake wa kufanya harusi yake katika usiri mkubwa na bila kufanya sherehe kubwa kama wanavyopenda kufanya mastaa wengi.



Banky W kabla ya kufunga ndoa na mpenzi wake Adesua Etomi, aliwahi kunukuliwa akisema kuwa yeye sio muumini wa kupenda kufanya sherehe kubwa akioa na angependa ikitokea akaoa atafanya sherehe ndogo na ya kawaida lakini itakuwa private.

Hivyo Banky W ametumia ukurasa wake wa instagram na kufunguka kwa wale wanaokosoa uamuzi wake wa kufanya hivyo Naona watu wanavyotaka kukosoa kwa comment yangu iliyopita kwa kusema mimi sio muumini wa kupenda kufanya sherehe za mbwembwe na mambo mengi, yamkini nimeonekana mnafiki”



“Bado mimi sio muumini wa kufanya sherehe kubwa za harusi na kama ingekuwa matakwa yetu harusi yetu ingekuwa ya kimya kimya na ndogo kama ingewezekana lakini tulijifunza mapema kuwa ndoa sio kitu cha watu wawili kuungana bali ni muunganiko wa familia hususani wazazi walikuja na matakwa yao”- Bank W





Aunt Ezekiel azua gumzo na maswali “dahh! Wanaumeā€¯

Chanzo: millardayo.com