Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeuri ya pesa! Uwoya anatembea na Dola, Shilingi ni nzito

Uwoyaaa Jeuri ya pesa! Uwoya anatembea na Dola, Shilingi ni nzito

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Irene Uwoya; ni mwanamama mkali mbele ya kamera za Bongo Movies ambaye mpambe wake, Aristote anasema sasa yupo kwenye listi ya mabilionea wanawake wachache nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Aristote, Uwoya amemueleza kuwa, huwa anatembea na dola pekee kwa sababu shilingi zina uzito.

“Irene ni bilionea mwanamke, huwa anatembea na dola, anakuambia shilingi zina uzito.

“Pia Irene anasema anahitaji maadui wapya kwa sababu maadui wa zamani wameshakuwa washkaji zake,” anasema Aristote.

Jamaa huyo ambaye ni mfanyabishara wa nywele za wanawake jijini Dar anasema kuwa, miongoni mwa mambo ambayo yanamshangaza ni pale ambapo Uwoya alikwenda visiwani Zanzibar kula chakula cha jioni ambapo alitumia dakika 15 tu kisha akarejea Dar.

“Yaani fikiria mtu ameenda Zanzibar akakaa dakika 15 kisha akarejea Dar es Salaam baada ya kula tu, hiyo kama siyo kufuru ni nini?” Anahoji Aristote akisisitiza kwamba Uwoya ana pesa ndiyo maana yeye na kampani yake wanainjoi maisha kwa kula bata ndefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live