Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jennifer Mgendi: Maumivu ya kufiwa na mume hayabebeki

Mgendiz Jennifer Mgendi

Sun, 8 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JENNIFER MGENDI; ni Staa mkubwa wa Muziki wa Gospel nchini Tanzania na mwigizaji mkali wa Bongo Movies ambaye amekumbusha mashabiki wake machungu.

Mgendi amekumbushia maumivu aliyoyapata baada ya kufiwa na mumewe, Dk Job Chaula yapata miaka miwili iliyopita ambapo leo Mei 7, 2022 amesema;

“Miaka miwili ni kama jana. Alipofariki baba yangu, Mzee Mgendi nilihisi mtu amenikata upanga kichwani na kunipasua vipande viwili na nilidhani hakuna maumivu yazidiyo hayo.

“Kumbe maumivu ya kufiwa na baba mwema kabisa hayakuwa lolote mbele ya maumivu ya kufiwa na mume (inategemea na mume mwenyewe sasa kama ni wale pasua kichwa ni jambo jingine maana nishakutana na wanawake kadhaa wanasema wananionea wivu kufiwa na mume)!

“Lakini kwa huyu wangu Dr Job Asheri Chaula (bilionea wa upendo) nilihisi moyo umepigwa bomu na kupasuka vipande 1,000,000.

“Namshukuru sana Mungu kwa kuendelea kuvikusanya vipande vya moyo wangu hadi sasa kuna vipande vingi havijapatikana, ila namshukuru Mungu mno kwa neema yake toshelevu.

“Maumivu kwenye nafsi yalikuwa makali mno, ila Mungu ashukuriwe maana yeye amejeruhi kisha yeye anaganga mwenyewe (Hosea 6). Nawashukuru wote wanaoniombea na kunitia moyo kwa hali na mali zao Mungu awabariki sana. Tuimbe: ATI TWONANE MTONI?”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live