Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jennifer Lopez afuta ziara yake ya Marekani

Jennifer Lopez Afuta Ziara Yake Ya Marekani Jennifer Lopez afuta ziara yake ya Marekani

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jennifer Lopez amesema "amesikitika" sana baada ya kufuta tamasha lake la moja kwa moja nchini Marekani.

Kampuni ya utoaji tikiti ya Live Nation ilitangaza Ijumaa kuwa ziara ya majira ya joto ya 2024 imefutwa, ikisema mwimbaji huyo "anachukua likizo kuwa na mtoto wake, familia na marafiki wa karibu".

Akiwahutubia mashabiki kupitia jarida lake, mwimbaji huyo aliandika: "Nimehuzunika sana na kukukatishwa tamaa."

Live Nation iliwahakikishia mashabiki katika taarifa kwamba watarejeshewa pesa zao.

Ziara hiyo ilikuwa imepangwa baada ya albamu ya tisa ya Lopez, ‘This Is Me... Now’, ambayo ilitolewa miaka 20 baada ya albamu yake maarufu, This Is Me... Then. Ni albamu ya kwanza ya mwimbaji huyo kwa miaka mitano.

Akiwaandikia mashabiki, Lopez alisema: "Singefanya hivi ikiwa singehisi kuwa ni muhimu.

"Nawaahidi nitawafanyia kitu kizuri na tutakuwa pamoja tena. Nawapenda sana. Mpaka wakati mwingine."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live