Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Jeff Bezos ampiku Elon Musk kwa utajiri

Elon Jeff Mz.png Jeff Bezos ampiku Elon Musk kwa utajiri

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeff Bezos amempiku Elon Musk na kuwa mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 200,Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miezi tisa, Elon Musk sio mtu tajiri zaidi duniani.

Musk alipoteza wadhifa wake kwenye orodha ya watu tajiri zaidi ya"Bloomberg Billionaires Index" kwa Jeff Bezos baada ya hisa zaTesla Inc kushuka kwa asilimia 7.2 siku ya Jumatatu. Musk sasa ana utajiri wa dola bilioni 197.7 huku Utajiri wa Bezos ni $200.3 bilioni.

Ni mara ya kwanza kwa Bezos, mwanzilishi wa Amazon.com Inc kuwa juu katika orodha ya Bloomberg ya watu tajiri zaidi tangu 2021, Pengo la utajiri kati ya Musk na Bezos lilikuwa pana kwa dola bilioni 142, limekuwa likipungua huku hisa za Amazon na Tesla zikipishana.

Hisa za Amazon zimeongezeka mara mbili tangu mwishoni mwa mwaka 2022 huku hisa zaTesla zikiwa chini karibu 50% kutoka kilele chake cha 2021 .Sababu ya kushuka ni baada ya data ya awali kuonyesha usafirishaji kutoka kiwanda chake huko Shanghai kushuka hadi kiwango cha chini zaidi kwa mwaka mmoja. Wakati huo huo, Amazon ikikuza ukuaji wake na ubora wa mauzo mtandaoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live