Ikiwa imepita zaidi ya Miaka 5 tangu rapa Bolionea Jay-Z kuachia album yake ya 4:44 huenda mwaka huu mashabiki zake wakafurahia ladha tamu yamuziki wake pia kwani rapa huyo ameripotiwa kuwa huenda akaachia album yake mpya mwaka huu.
Kwa mujibu wa muongozaji wa video (Director) @hidjiworld ametudokezea habari hizi njema za ujio wa Album ya Jay-Z kupitia ukurasa wake wa Instagram pale kwenye Instastory huku ikionyesha kuwa nyimbo hizo za album huenda zikaja na video zake tayari.
Album ya mwisho kutoka kwa rapa Jigga ilikuwa ni 4:44 iliyotoka mwaka 2017 kwa hiyo huenda album hii ikaja na baraka nyingi na kukata kiu kwa mashabiki wa Hov.