Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Z atamba kuwa hana mshindani stejini #VERZUZ

Jayzeeeepic Data Jay Z aweka wazi kuwa hana mshindani

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia Twitter Space wakiwa live kwenye mazungumzo na mwanamuziki Alicia Keys wakati akisherehekea mafanikio ya albamu yake mpya “Keys” na marafiki kupitia mtandao huo, Rapa Jay Z amejitapa kwa kusema “hakuna rapa yeyote anayeweza kusimama naye kwenye jukwaa la Verzuz na kushindana naye kwenye Verzuz.”

Jay Z amekuwa msanii mwenye jina kubwa ambaye wasanii wengi wamekuwa wakiomba kufanya pambano la kimuziki na rapa huyo Verzuz.

Wiki moja iliyopita rapa Rick Ross aliweka rekodi akisema kuwa anaweza kushinda kwenye Verzuz dhidi ya Jay Z na kuwa walau huyo ndio msanii wa hadhi yake.

Kulingana na kauli ya Jay Z ni kuwa hakuna mtu mwenye nafasi ya kufanikiwa watakaposimama kwenye Verzuz.

Pamoja na kutamba kuwa hayupo wa kushindana naye Jay Z Pia aliendelea kwa kupongeza wazo la Verzuz na jinsi jukwaa hilo linavyotoa nafasi kwa wasanii.

Verzuz ni program maalumu iliyoanzishwa na watayarishaji mahiri wa muziki kutoka nchini Marejani Swizz Beats na Timberland ambayo hurushwa live kupitia Verzuz Tv.

Hii ni Program iliyotambulishwa katika kipindi cha janga la Covid19 kama Virtul Dj and Rap battle.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live