Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Z ashinda kesi ya Bilioni 16

Jigga Jay Z Jay Z ashinda kesi ya Bilioni 16

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jay-Z ndio ule mfano wa mwenye nacho huongezewa, Rapa huyo ameripotiwa kuwa ameshinda rufaa ya Kesi yake dhidi ya Kampuni ya manukato maarufu kama Parlux.

Mwaka 2016 Kampuni hiyo ilimshtaki Jay-Z kwa kushindwa kufuata baadhi ya makubaliano hivyo kutafsiriwa kama amevunja mkataba. Walienda Mahakamani na kudai fidia ya ($67 million) zaidi ya TSh. Bilioni 158.

Jay-Z baada ya kupokea shtaka hilo, na yeye alizunguka na kuifungulia mashtaka kampuni hiyo kwa madai kwamba hawakumpa taarifa isiyo sahihi kuhusu afya ya Kampuni Kifedha ikiwemo kushindwa kumlipa Mirabaha (Royalties) aliyokuwa anadai kama sehemu ya Ushirikiano wao.

Shauri hilo la mwaka 2021 limeishuhudia Mahakama ikimpatia ushindi Jay-Z na kutupilia mbali madai ya Parlux, ambapo sasa watatakiwa kumlipa Jay-Z kiasi cha ($6.8 million) zaidi ya TSh. BILIONI 16 kama madeni ya Mirabaha ambayo hawakuwahi kumlipa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live