Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Moe aliwaumbua wanasayansi, akawasuta wahenga

Jay Moe Mchopanga Jay Moe aliwaumbua wanasayansi, akawasuta wahenga

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanabiolojia walipima. Wakaripoti kuwa mbuyu huchukua miaka 15 - 20 kupevuka. Wastani wa ukuaji ni mm 8 miezi mitatu. Fasta ni meta 1 kwa mwaka. Wahenga wakabariki vipimo. Wakatambulisha shortcut formula: "Mbuyu ulianza kama mchicha."

Homeboy wa K'Nyama na Sinza, Jay Moe, akawaita kati wanasayansi na wahenga, akawaambia "tupinge".

Track "Majukumu" ilikomba odds zote. Buza mpaka Mkongoro. Malampaka hadi Nangulukulu. Usoke na Hedaru. Maskani na baraza zote zilifall in love kwa Jay Moe.

Wahenga na wanasayansi walipigwa KO. Jay Moe alithibitisha yeye ni mbuyu kamili kwa strain moja kama solo redioni. Mibuyu mingine ruksa kuanza kama mchicha. Hapana kuilinganisha na The Superman.

Beloved students and scholars; kwenye pitapita zako kama utaulizwa "who is Jay Moe?", usicheleweshe jibu: "Jay Moe ni mbuyu wa kipekee kwenye sanaa Tanzania." Kipindi cha msako wa breakthrough ya soko la filamu Tanzania, Jay to the Moe, alionekana ni trump card.

Jay Moe alikuwa mhusika muhimu kwenye movie ya Girlfriend ambayo ilitengeneza mpenyo wa soko la filamu Bongo. Kijana wa saluni lakini sio mnyonge mbele ya watoto wa kishua, rafiki wa TID, mwenye kipaji cha muziki.

AY, Mfalme Chizi GK, Monalisa, Nina na Sauda Simba ni amongst others, waliotisha kunako Girlfriend.

Jay Moe aliingiza beti mbili kwenye ngoma "Girlfriend", iliyosimama kama soundtrack ya movie. Vipande vingine vilimalizwa na Mnyama Mkali TID.

So now you know; Jay Moe ni mbuyu kwenye Bongo Fleva ambaye hakufuata formula ya kuanza kama mchicha. Moreover, ni mwanamapinduzi wa soko la filamu Tanzania.

Ukiniuliza Jay Moe ni nani? Nageuza shingo. Napress-play "Tingisha". Acha tutingishe kama kiberiti. Je, njiti zimo?

Zaidi ya miongo miwili kwenye game. Akaunti yake ina takriban hits dozen mbili. Kwa kuheshimu hilo, Bongo Flava Honors, inakwenda kumpa heshima kamili Jay Moe. Atatunukiwa tuzo ya maisha yenye mafanikio kwenye Bongo Fleva. Halafu, atagonga dozen mbili ya hits zake kwa live band.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live