Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Melody ametangaza kuacha muziki!

Msanii Wa Bongo Flava Jay Melody Ametangaza Kuacha Muziki!.png Jay Melody ametangaza kuacha muziki!

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Radio Jambo

Msanii anayefanya vizuri kwa mizki ya Bongo Fleva, Jay Melody ametangaza kuacha masuala ya utunzi na uimbaji wa muziki.

Katika kile kilichowashangaza mashabiki wake wengi ambao wamempa mapokezi mazuri katika kipindi cha kama miaka 3 tangu nyimbo zake zilivyotusua, Melody alipeleka katika instastory yake na kuandika ujumbe mfupi akisema;

“Ninaacha kuimba muziki!” na kumalizia na emoji ya kushukuru.

Hata hivyo haijulikani ni nini kimemsibu msanii huyo hadi kufikia hatua ya kutamka uamuzi huo lakini pia wengine walihisi huenda ni kibao kipya anawatayarishia mashabiki wake na tamko hilo lenye utata ni njia moja ya kuamsha popo zao.

Msanii huyo mwaka huu amekuwa mnyamavu sana katika kuachia miziki pendwa kwa mashabiki wake ikilinganishwa na mwaka jana, mwaka ambao ulisisima jina lake mioyoni mwa mashabiki wengi wa mashairi ya Bongo Fleva.

Kwa kuangalia katika chaneli yake ya YouTube, Jay Melody aliachia kibao cha mwisho miezi minne iliyopita, ikiwa ni audio kisha mwezi mmoja baadae akaachia lyrics za kiingereza cha wimbo huo ‘Mbali Nawe’ na tangia hapo amekuwa mnyamavu kwa kuwakaushia mashabiki waliokuwa wanasubiri Video.

Chanzo: Radio Jambo