Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Melody afunguka kuhusu undugu na Z Anto

Jay Melody Z Anto Asd Jay Melody afunguka kuhusu undugu na Z Anto

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Sharif Said Juma maarufu kama Jay Melody amesema kuwa hana undugu wowote na legend wa muziki huo, Ally Mohamed maarufu kama Z- Anto kama wengi ambavyo wamekuwa wakidai kuwa ni mtu na kaka yake.

Jay amesema kuwa anamchukulia Z Anto kama kaka yake kutokana na kwamba alimtangulia kwenye muziki na kufanya vizuri kiasi cha kumvutia hata yeye.

“Watu wanasema tumefanana lakini Z Anto sio ndugu yangu kabisa. Sina undugu naye hata baadhi ya moments nilivyokuta naye pale THT watu walikuwa wanasema ni ndugu yangu.

“Mimi namchukulia kama Brother na msanii ambaye nimemuona zamani na Hits zake kama Binti kiziwi zilizotamba mitaani,” amesema Jay Melody.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live