Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Melody: Nampenda Paula

KUSAH NA PAULA Jay Melody: Nampenda Paula

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody amefunguka wazi kuhusu picha ya mwanadada Paula Kajala ambayo aliiposti juzi katika ukurasa wake wa Instagram na kisha baadae kuifuta.

Akizungumza katika kipindi cha Refresh cha Wasafi, Melody amesema kwamba aliposti picha mbili na wala hakuwa na maana kwamba anammezea kimapenzi Paula bali anamkubali tu kama anavyowakubali mashabiki zake wengine.

“Kama ulikuwa makini sana utagundua kulikuwepo na picha mbili. Picha moja ni ya kwangu nimepiga na ua kichwani na ya pili ni ya Paula. Mimi nampenda kama miongoni mwa watu wengine ninavyowapenda.

"Namuona picha zake nzuri na ile niliyoipakia niliipenda lakini maelezo niliyofuatisha kwenye picha zile hayahusiani na picha yake,” Jay Melody.

Msanii huyo alisema kwamba wala hawana ukaribu wowote na Paula na hata hawajawahi kuwa na maongezi ya aina yoyote na pia kusema kwamba kilichomfanya kuifuta picha ile ni baada ya kuona maoni ya watu na akaona haina haja kumtengenezea mazingira ya msongo wa mawazo mtoto wa watu na ndio maana akaizamisha.

“Sema tu nilivyoona yale maoni ya watu nikaona sina haja ya kumtengenezea mtoto wa watu msongo wa mawazo ndio maana nikaitoa maana pale walikuja hadi wajomba zake. Mimi naheshimu sana watu, hata Paula nampenda, namuona anapiga picha kali ndio maana nikaiposti tu,” Jay Melody.

Inasemekana Paula kwa sasa ni jimbo liko huru baada ya penzi lao na msanii Rayvanny kuingia mchangani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live