Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jason Derulo naye akumbwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono

Jason Derulo (19).jpeg Jason Derulo naye akumbwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Marekani ‘Jason Derulo’ anakabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kijinsia, kutoka kwa Binti ambae ni mwimbaji aliyemwondoa kwenye lebo yake baada ya kukataa matamanio yake ya ngono.

NBC News, inaripoti kwamba binti ‘Emaza Gibson’ amewasilisa kesi hiyo Oktoba 5, mwaka huu ambapo ametoa madai hayo. Ambapo anakiri kupoteza mapato ya kazi yake baada yakufurushwa.

“Sijalipwa ujira wangu, nimepoteza mapato ya muziki wangu, fidia yakusitishiwa mkataba na kulolipwa mirabaha” amefunguka mwanadada huyo kidosho ‘Emaza’.

Mbali na madai ya unyanyasaji wa kijinsia, ambapo anadai kwamba aliahidiwa dili la rekodi ikiwa tu angelala na “Derulo”, na kumtisha kuwa endapo akimkataa basi atasitisha dili hilo.

“Jason Derulo sio tu kwamba alivunja mkataba, lakini pia alitoa vitisho vya usalama wake wakati wa ushawishi usio wa kawaida wa nfono dhidi ya msichana huyu ambaye anajaribu kuingia kwenye tasnia ya muziki ambavyo vilikuwa vya kuudhi na haramu” amefunguka ‘Ron Zambrano’ ambae ni Wakili wa binti ‘Ezama’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live