Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Januari 1, 2024 idadi ya watu Duniani itafikia bilioni 8+

Population Dunia(2).jpeg Januari 1, 2024 idadi ya watu Duniani itafikia bilioni 8+

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya Watu duniani imeongezeka kwa jumla ya Watu milioni 75 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo ongezeko hilo litapelekea idadi ya Watu siku ya mwaka mpya January 01,2023 kufukia zaidi ya Watu bilioni 8 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Hesabu ya Watu Marekani.

Mtandao wa VOA Swahili umeripoti kuwa kiwango cha ukuaji duniani kote mwaka uliopita kilikuwa chini ya asilimia moja ambapo forget mwanzoni mwa mwaka 2024 Watoto wanaozaliwa 4.3 na vifo viwili vinatarajiwa duniani kote kila sekunde kwa mujibu wa takwimu za sensa, kiwango cha ukuaji wa Marekani katika mwaka uliopita kilikuwa asilimia 0.53 karibu nusu ya takwimu ya kimataifa.

Marekani imeongeza Watu milioni 1.7 na kufikia siku ya mwaka mpya itakuwa na Watu milioni 335.8, huku taarifa zikizema kama kasi ya sasa itaendelea hadi mwisho wa muongo basi miaka ya 2020 inaweza kuwa muongo wenye kasi ya polepole zaidi ya ukuaji katika historia ya Marekani na kuweka kiwango cha ukuaji wa idadi ya Watu chini ya asilimia 4 kwa kipindi cha 2020 hadi 2030.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live