Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Jane: Ukitaka nikuzalie nilipe Tsh milioni 786

Jane Ms Jane: Ukitaka nikuzalie nilipe Tsh milioni 786

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo huyo kwa jina la Jenny (23) ameibua minong'ono baada ya kuweka wazi kuwa hana mpango kabisa wa kuzaa ila mwanaume akitaka ambebee mimba na kumzalia mtoto ni lazima kila mwaka alimlipe £250,000 ambazo sio chini ya shilingi milioni 786 za Tanzania.

Pesa hizo zitakuwa gharama za yeye kufanyiwa therapy, kumlipa mwalimu binafsi wa mazoezi ya viungo (personal gym trainer), na mahitaji ya mtoto.

Jenny anayeishi London, Uingereza anasema kuwa mama ni kitu chenye thamani kubwa na inahitaji mtu kujitoa muhanga kubeba kiumbe mwilini na kukileta duniani hivyo yeye hafanyi suala hilo bure kwa mwanaume, anasema yeye hakuumbwa kuja kupata tabu.

Jenny ameeleza kwamba kuna wakati alimtaka daktari aliondoe tumbo lake la uzazi sababu hana mpango wa kuzaaa kabisa katika maisha yake.

Amesema kabla hajabeba mimba ni lazima yawepo makubaliano rasmi ya kisheria kuhusu yeye kulipwa shilingi milioni 786(£250k) za matunzo kila mwaka Anasisitiza kamwe hawezi kubeba mimba kabla ya ndoa ni lazima wafunge ndoa kwanza ndio atabeba mimba.

Amesema kabla hawajafunga ndoa na kabla hajabeba mimba ni lazima pia yawepo makubaliano ya kisheria kuhusu kutokwepo usaliti ndani ya ndoa( infidelity clause), hatovumilia mwanaume msaliti hata kama kaolewa sababu hataki kuubebsha mwili wake mzigo wa maumivu wala hataki kujiletea matatizo ya afya ya akili ya kusabaishwa na mwanaume ili hata ndoa ikivunjika kwasababu ya usaliti kuwepo na fidia kisheria.

Pia lazima awekewe mfanyakazi wa kuangalia nyumba akiwa mjamzito na pia akijifungua awekewe mtalaamu maalum wa kumsaidia mama aliyejifungua, anasema yeye hajui wanawake wanaopika, kufanya usafi na kwenda kazini wanawezaje ila kwake itakuwa ngumu.

Amesema akishajifungua itategemea na uzazi umeleta mabadiliko gani mwilini mwake hivyo mwanaume atahitajika kulipia gharama za sajari arekebishwe tumbo lake likae sawa la kuvutia kama mwanzo na pia matiti yake yafanyiwe sajari yavutie kama mwanzo kwasababu aliyetaka mtoto ni mwanaume siyo yeye.

Kabla ya kujifungua lazima apelekwe mapumziko nje ya nchi akafurahie kwa kutarajia kuleta kiumbe duniani(babymoon). Na, pia lazima apewe zawadi ya gari au nyumba kwa kuleta kiumbe duniani (luxury push present).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live