Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jane Fonda anataka mume wa miaka 20

Jane Fonda Jane Fonda anataka mume wa miaka 20

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jane Fonda (85) mwigizaji maarufu Marekani ambaye yupo singo, katika mahojiano mapya alipoulizwa kuhusu kuwa katika mahusiano katika umri alionao sasa.

Amejibu kwa kusema anajisikia aibu kwa anachoongea ila kama ni lazima awe katika mahusiano katika umri alionao, atachagua mwanaume mwenye miaka 20 ndie awe mpenzi wake.

Alipoulizwa kwa nini mwanaume mwenye miaka 20, amejibu kwa sababu hapendi ngozi kongwe zilizozeeka, ambapo aliibua vicheko kwa mtangazaji na producers wa kipindi ingawa Jane yeye alibaki kuwa serious.

Jane ambaye alishaingia kwenye ndoa tatu na kujaaliwa watoto watatu wenye miaka 55, 54 na 49, hata hivyo kwa muda mrefu ameamua kuwa single akionekana hana nia tena ya kuwa katika mahusiano tofauti na mitazamo ya wengi kuwa uzeeke ukiwa na mwenza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live