Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamafest yasogeza mbele mechi Taifa Stars, Sudan

76750 Pic+stars

Sun, 22 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Sababu za mchezo wa kati ya Taifa Stars ya Tanzania dhidi ya Sudan kusogezwa mbele kutoka saa 10 jioni hadi saa 1 usiku zimetolewa kuwa ni uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest).

Uzinduzi huo unafanyikiwa leo Jumapili Septemba 22, 2019 na Makamu wa Rais Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi kati ya Taifa Stats na Sudani ya kusaka nafasi ya kufuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan).

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili, Mkurugenzi wa michezo, Yusufu Single amesema mechi hiyo iliyokuwa ichezwe saa 10 jioni sasa itachezwa saa 1 usiku.

Single amesema wameamua kufanya hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo kwa Taifa na kueleza wanatarajia litaisha saa saba huku shughuli nyingine zikihamia uwanja wa Uhuru.

"Kwetu hili tamasha ni muhimu pia kwa Taifa kama ilivyo mechi ya Taifa Stars na Sudan, hivyo tumeona tusogeze mbele mechi hii wananchi wasisite kuja kuishuhudia kwani ratiba zote zipo sawa kama zilivyopangwa," amesema.

Pia Soma

Advertisement
Akizungumzia  tamasha hilo, Mratibu wa Jamafest Tanzania, Joyce Fisoo amesema tamasha hilo lilianza miaka minne iliyopita kwa kuanzia Rwanda, Kenya, Uganda na sasa ni Tanzania.

Fisoo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kwa siku nane ambapo litakuwa likifanyika ili wapate kujionea tamaduni mbalimbali zinazoonyeshwa.

Tamasha hilo lenye lengo la kutangaza tamaduni za nchi za Afrika Mashariki, limeanza jana Jumamosi na litafika kilele Septemba 28, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz