Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa atinga kwenye harusi yake akiwa ndani ya jeneza

JENEZA Bn Jamaa atinga kwenye harusi yake akiwa ndani ya jeneza

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Video fupi ya mtandaoni iliyoshirikiwa na @tobz88 imeonyesha wakati bwana harusi akizua kisanga kufika kwenye harusi yake akiwa ndani ya jeneza.

Wakati wageni na bibi harusi mrembo walikuwa wakisubiri, wapambe wake waliwasili wakiwa wamelibeba jeneza jamaa akiwa ndani.

Katika kanda ya TikTok iliyosambaa kwa kasi, baada ya kuweka jeneza chini nyuma ya bi harusi, walilifungua, na mwanaume huyo akatoka kwa upole. 

Harusi hiyo, ambayo ilifanyika kando ya mto, ilikuwa na wageni wengine waliokuwa wakipiga picha wakitumia simu zao ili kunasa matukio hayo ya ajabu.

Watu wengi waliotoa maoni yao kuhusu video hiyo walieleza kushangazwa na harusi hiyo isiyo ya kawaida. Wengine walisema kwamba kamwe hawatashiriki katika hafla kama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live