Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JamaFest yaja Bongo Tanzania

73402 Jamal+pic

Thu, 29 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tamasha kubwa la maonyesho ya sanaa ambayo hujumuisha nchi za Afrika Mashariki (JamaFest) litafanyika Septemba 21-28 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam nchini Tanzania.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Alhamisi Agosti 29,2019, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa tamasha hilo tangu lianzishwe mwaka 2011.

Amesema ili tamasha hilo livutie wanafanya mpango kuwashirikisha wasanii wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumuz na Saida Kalori.

"Tunataka makundi ya kisanaa yenye vitu vya kipekee ili yavutie, tutaongea na Saida Kalori na Diamond, hawa wana mashabiki wengi, tutataka waje ili kufanya tamasha livutie," amesema Dk Mwakyembe.

Amesema tamasha hilo ambalo huitwa Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival (JamaFest) kwa mara ya kwanza lilifanyika Rwanda mwaka 2013 na kuhudhuriwa na watu 17,500.

Amesema tamasha hilo ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili, lilifanyika kwa mara ya pili Kenya mwaka 2013 na kuhudhuriwa na watu 21,000.

Pia Soma

Uganda iliandaa tamasha hilo mwaka 2017 na kuhudhuriwa na watu 46,500 na sasa litafanyika Tanzania mwaka 2019.

"Hii ni sehemu pekee ya kutambulisha sanaa katika dunia. Masuala yote ya sanaa yanatakiwa kuja na kuonyesha dunia vivutio tulivyonavyo," amesema Dk Mwakyembe.

Amesema tamasha hilo limeanza kuvutia dunia nzima na ndio maana anataka Tanzania ijivunie na ikiwezekana kuvunja rekodi ya matamasha yote yaliyopita

Chanzo: mwananchi.co.tz