Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji wa audition alitaka nifanye naye mapenzi - Anitha wa Juakali

Jua Kali, Anita Anitha wa Juakali

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa Tamthilia ya Juakali, Anita amefunguka kuwa wakati akiianza safari yake ya Usanii amewahi kwenda kwenye mchujo wa kutafuta Waigizaji (audition), lakini mmoja kati ya Majaji wa zoezi hilo alimtongoza na kumueleza kwamba kama anataka nafasi hiyo ni lazima kwanza akubali kufanya nae mapenzi.

"Nakumbuka miaka mitatu nyuma nilienda kwenye audition ya tamthilia kubwa tu, nilivyofika nikaigiza vizuri lakini yule baba akaniambia unaweza lakini tutakuita, baadae alinitafuta kupitia namba yake binafsi akaniambia mimi ni jaji nilikuwa pale kwenye audition nataka kukutana na wewe"

"Aliongea maneno mengi mabayamabaya, lakini nilienda kusikiliza, baadae akaniambia una nafasi leo usiku uje sehemu fulani tuweze kuonana mimi na wewe, nikamwambia usiku hapana kwani hatuwezi tunaongea hapahapa, akaniambia kama huwezi kuja usiku basi, kuanzia hapo sikupewa kazi akaniambia kiwango changu bado sijachangamka.

"Lakini aliponiona kwenye Juakali mara ya kwanza alinitafuta akaniomba msamaha, akasema nilikudharau sana sikutegemea kama ungekuja kufanya kazi kubwa kama hii naomba unisamehe," Anita wa Juakali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live