Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jada, Will Smith walitengana tangu 2016

Jada X Smith Jada, Will Smith walitengana tangu 2016

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji na mtangazaji kutoka nchini Marekani #JadaSmith ameweka wazi kuwa yeye na mume wake Will Smith ambaye pia ni muigizaji walitengana kwa siri miaka 7 iliyopita huku akieleza kuwa hawana mpango wa kupeana talaka.

Kufuatia mahojiano yake leo asubuhi na NBC News baada ya kuulizwa kuhusu hali yao ya ndoa alieleza kuwa yeye na mumewe walitengana kwa siri toka mwaka 2016 licha ya kujaribu kurudisha uhusiano wao lakini haikuwezekana.

Jada alifichua kuwa hata wakati wa Tuzo za Oscar 2022, Will alipompiga kibao Chris Rock, walikuwa wametengana kwa miaka sita.

Hata hivyo Jada ameeleza kuwa kwa sasa bado wanaendelea kutafakari kuhusu kutengana kwao kwa sababu wamekuwa wakipeana support huku akiamini kuwa bado wana upendo wa dhati kati yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live