Muigizaji maarufu duniani, Jackie Chan aliwashangaza watu wengi kwa kusema kwamba mtoto wake, Jaycee Chan hataambulia hata mia yake kwenye utajiri wake na hivyo apambane kwenye kujitengenezea mali zake.
Muigizaji maarufu duniani, Jackie Chan aliwashangaza watu wengi kwa kusema kwamba mtoto wake, Jaycee Chan hataambulia hata mia yake kwenye utajiri wake na hivyo apambane kwenye kujitengenezea mali zake. Jack aliweka wazi kuwa anapanga kuacha zaidi dola milioni 400 (Tsh bilioni 935.600) kama msaada kwa wenye uhitaji na sio kwa mtoto wake kwani anaamini kama ana uwezo anaweza kujitengenezea pesa zake mwenyewe na kama hana huo uwezo basi hata akimuachia fedha hizo atazipoteza tu.