Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JCB aponda ma-dj na watangazaji wanaoendekeza rushwa

1031 19367924 1055330581233716 7420416032386318336 N TZW

Thu, 4 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki hip hop wa Bongo, JCB amekosoa mfumo ambao unadaiwa kuwepo katika Bongo Flava ambao ni wasanii kulipa fedha ili kupata interview na nyimbo zao kuchezwa katika vyombo vya habari hasa redio na runinga.

Rapper huyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kitu hicho si kizuri kwani licha ya kuua muziki inaweka uzibe kwa wasanii wachanga.

“Hiyo kitu ni zuluma, ni utapeli yaani vitu ambavyo havitakiwa kuwepo na ni kweli hiyo system ipo Tanzania muda huu, nasikia ukitaka interview utoe hela, ili wimbo wako uchezwe utoe hela,” amesema JCB.

JCB ameongeza kuwa kutokana na tabia hiyo kuanza kushamiri ndio sababu miaka ya hivi karibuni hakuna msanii underground aliyetoka na kufanya vizuri bali wanaosikika ni wale wale ambao tayari wanajuana na baadhi ya watu katika vyombo vya habari.

Chanzo: bongo5.com