Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JB ndiyo mwigizaji bora wa kiume Tanzania - Manara

Manara Jb JB ndiyo mwigizaji bora wa kiume Tanzania - Manara

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mdau wa masuala ya soka na burudani nchini, Haji Manara amesema kuwa staa wa sanaa ya maigizo nchini, Jacob Steven 'JB' ndiye msanii Bora wa Bongo Movies kwa sasa.

Manara amesema hayo mara baada ya JB kupokea tuzo yake ya @hapa.awards aliyoshinda hivi karibuni nchini Marekani na kukabidhiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro.

JB na Phina wameshinda tuzo za @hapa.awards zilizoandaliwa na Mtanzania Mzalendo Mawwiny Cassey, JB alishinda tuzo ya Best Bongo Movie Actor, huku Phina akishinda tuzo ya Best Female Bongo Flavour East Africa.

"Kwangu mimi JB ni Muigizaji bora wa Filamu wa kiume wa muda wote Tanzania, juu yake yupo King Majuto. Hajapewa tu heshima yake anayostahili na Watanzania kwakuwa nchi hii hasifiwi mtu hadi afe na hapo ndipo tutakapoleta ngonjera zetu.

"Hivi Marehemu Kanumba heshima tuliyompa alipofariki inalingana na alipokuwa hai? Hatukujua yeye ni nani katika sanaa kwa ukubwa wake lakini alipolala chini tu nchi ilizizima na hekaya toka kila pembe zilirindima.

"Hatuna khulka ya kusifiana tukiwa hai na tunaweza kumuonea kijicho JB hata kwa posti hii tu, lakini huo ndio ukweli wangu, JB ndio Mwigizaji bora wa Filamu kuwahi kuzaliwa Tanzania.

"Wengine hatungojei kutoa sifa mbele ya jeneza, huyu ni mwamba hasa katika eneo lake, ni kweli anaudhi sana sometimes kwa kupenda kula kupita kiasi, wali ndani ya kusadolini unaisha hapo, lakini ndiyo top katika film industry Tanzania," amesema Haji Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live