Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JB apokea tuzo aliyotunukiwa Marekani

Jb Tuzooo JB apokea tuzo aliyotunukiwa Marekani

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amewakabidhi tuzo Wasanii Jacob Stephen (JB) na Saraphina Michael 'Phina' walizoshinda kutoka nchini Marekani.

Wasanii hao wameshinda tuzo za @hapa.awards zilizoandaliwa na Mtanzania Mzalendo Mawwiny Cassey, JB alishinda tuzo ya Best Bongo Movie Actor, huku Phina akishinda tuzo ya Best Female Bongo Flavour East Africa.

Waziri Ndumbaro amewakabidhi tuzo hizo wasanii hao na kusema amefurahi tuzo kufanyika Marekani, lakini wamepata wasanii kutoka Tanzania.

Waziri Ndumbaro amesema; “Tuna kila sababu ya kuwapongeza kwa tuzo zao. Kuna muda mwingine kunakuwa na ugumu wa kweli, muda mwingine kunakuwa na ugumu wa kutengeneza.

“Lakini pia tunatambua na tuzo za wadada zetu wawili Lady Jay Dee na Wema Sepetu, lakini kubwa tumpongeze Mawwiny, Diaspora wa namna hii lazima tumtambue na tumtangaze.

“Naomba tumtambue huyu kama Balozi wetu na atakapokuja Tanzania tumkabidhi Rasmi Ubalozi,” alisema Waziri Ndumbaro.

JB alisema tuzo hiyo kwake ni kubwa na ameanza Maigizo tangu mwaka 1997, lakini hajawahi kushinda tuzo ya namna hiyo.

“Hii kwangu ni kubwa sana. Nawashukuru Serikali katika kufanya nao kazi pamoja. 2016 tulipata dhoruba Bongo Movie na mfumo wa kazi zetu ulianguka na mwaka 2017 tulisimama tena, lakini kubwa nawashukuru Azam Tv (Sinema Zetu) na hii tuzo pia ni yenu.

“Nawashukuru na wasanii wenzangu nilioshirikiana nao. Naishukuru familia yangu maana kwa mwaka mzima kitanda changu nalala miezi 6,” amesema JB.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live