Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JAY-Z afuta ukurasa wake Instagram baada ya kufikisha wafuasi milioni 1.8

66280 Jayzeepic Pamoja na kupata wafuasi Milioni 1.8 JAY-Z afuta akaunti ya Instagram

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Jumanne, rapa Jay-Z aliushangaza ulimwengu wa burudani kwa kuanzisha akaunti ya Instagram. Ilikuwa hatua isiyotarajiwa kutoka kwa rapa huyo, ambaye mara chache hutumia mitandao ya kijamii.

JAY-Z alijiunga Instagram ili kuipromote filamu yake ya The Harder They Fall, ambayo ameshiriki katika kuitayarisha. Ingawa wengine wanaweza kuwa wakitazamia kile kingine angefanya na akaunti hiyo sasa hawatajua kamwe kwa sababu JAY amefuta ukurasa huo ndani ya masaa 24 bila kusema lolote.



Jaribio la kutembelea akaunti ya @jay-z kwenye Instagram linatoa ujumbe wa makosa, "Mtumiaji hakupatikana." Hii sio mara ya kwanza kwa Jay kufuta ukurasa wa Instagram haraka. miaka ya nyuma katika msimu wa joto wa 2015, alitengeneza akaunti chini ya jina @hovsince96 na ku-like picha yake na Michael Jackson.

Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la The New York Daily News, Jay alifuta ukurasa huo saa 14 baadaye. Hadi sasa Facebook na Twitter zimesalia kuwa akaunti zake pekee za mitandao ya kijamii.

Uamuzi wa Jay kufuta akaunti yake ya Instagram unakuja baada ya kutoa ushauri kwa watoto wenye "ndoto za kufanikiwa" wakati wa mahojiano mafupi na Jazzy, ripota wa Brooklyn mwenye umri wa miaka 11. "Jiamini mwenyewe, hata kabla ya mtu mwingine yeyote kukuamini," alisema. "Lazima uwe na imani kamili kama wewe. Unajiamini sana. Na jiamini tu wewe mwenyewe."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live