Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Issa Azam: Nikikuta Kiba na Mondi wanaungua moto namuokoa Simba

ISSA KIBA DIAMOND Issa Azam: Nikikuta Kiba na Mondi wanaungua moto namuokoa Simba

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa wa msanii Diamond Platnumz, Issa Azam amesema ikitokea akawakuta Diamond na Alikiba wanaungua kwa moto ataanza kumuokoa kwanza Diamond kisha Alikiba.

Issa ambaye amekuwa akijipambanua kuwa ni ndugu wa damu wa Alikiba, amesema hayo wakati akihojiwa na moja ya chombo cha habari huku akibainisha kuwa atafanya hivyo kumuokoa kwanza Diamond kwa sababu ndio fadhira pekee atakayompa kutokana na mambo makubwa aliyomfanyia katika maisha yake.

“Alikiba ni ndugu, lakini ikitokea Alikiba anaungua na moto, Diamond anaungua na moto nitamuokoa kwanza Diamond halafu ndio narudi kumuokoa ndugu yangu Alikiba sasa. Unadhani diamond nitamlipa nini tena shehe wangu?

“Pale itakuwa ndio fadhira yangu sasa kwa Diamond, nitamchukua Simba twende mwanangu, mwamba. Halafu ndio narudi kwa ndugu yangu Kiba namwambia twende. Kama Kiba ana vidonda nachukua pesa kwa Diamond nakwenda kumtibia, huoni kama nimetumia akili hapo?” amesema Issa Azam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live