Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Issa Azam: Nikifa Diamond asimamie msiba wangu, Kiba asikanyage kabisa

ISSA KIBA DIAMOND Issa Azam, Diamond na Kiba

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Issa Azam; ni ndugu wa msanii King Kiba ambaye alifanya kufuru ya karne kumtenga nduguye na kuungana na hasimu wake, Diamond Platnumz na sasa ameibuka na mapya tena.

Issa mwenye ukaribu na msanii Diamond Platnumz wengi wanamjua kama chawa wa WCB. Issa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akiliweka wazi suala hilo ikiwemo mshahara anaoupata kutoka kwa Diamond Platnumz kwa kazi yake ya uchawa.

Issa kwa kuwakomesha wanaomsema vibaya Simba, mshahara wake alisema ni mnono mno kwa mwezi.

Issa anasema kwamba mshahara wake kutoka kwa Diamond ni mara nne zaidi ya Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mimi mshahara yangu nikiungaunga, ni mishahara minne ya Mbunge,” anasema Issa. Issa anaonesha chuki yake dhidi ya King Kiba na wanafamilia wengine kwa kile anachosema kwamba aliwachukia kwa kutaka kumuua Diamond kwa kumpiga mawe ila wakashindwa.

Issa anaweka wazi kwa mara nyingine tena kwamba ikitokea amefariki leo hii, basi watu wa familia ya King Kiba wasijaribu kufika kwenye msiba wake kumzika.

“Mimi leo hii nikifa, kwenye kaburi langu nisiwahi waona watu hao. Msiba wangu utasimamiwa na watu wa Wasafi. Msimamizi wa msiba wangu atakuwa Nasibu Abdul (Diamond Platnumz). Naomba Diamond anizike ili nife kwa furaha. Kiba asifike kabisa kwenye msiba wangu, hata kwangu asijaribu kufika,” anasema Issa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live