Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishaq: Sabra ni mjamzito na mimba ni yangu

Sabra Mjamzito Data Ishaq: Sabra ni mjamzito na mimba ni yangu

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Ishaq Mtoro ambaye ni mume wa msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Queen Darleen, ametoboa siri kwamba mke wake mkubwa anayetambulika kwa jina la Sabra ni mjamzito na mimba ni yake.

Sabra ambaye ni mke mkubwa wa mume wa msanii huyo, wamekuwa kwenye ndoa  kwa miaka sita sasa lakini hawakuwahi kubahatika kupata mtoto.

Hata hivyo wakati huko mitandaoni kukiwa na taarifa kuwa mwanamke huyo amebeba mimba ya mwanaume mwingine na tayari ameshamtwanga talaka.

Akizungumza leo Jumanne Februari 9,2020 katika kipindi cha mashamsham kwenye redio ya Wasafi, aliondoa utata huo na kueleza kuwa ni kweli Sabra ana mimba na mimba ni yake wake.

Akijibu kwa kifupi swlai hilo amesema’Ni kweli Sabra ni mjamzito na mimba ni yangu”amesema Ishaq.

Kuhusu tetesi za kuachana na bimkubwa zinazoelezwa huko mitandaoni, Ishaq alikanusha na kueleza kuwa ni mwanamke ambaye hataraji kumuacha leo wala kesho kwa kuwa wametoka naye mbali na anajua thamani yake.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz