Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishaq: Sabra amesababisha Queen Darleen anijue

Ishaq Pic Data Ishaq: Sabra amesababisha Queen Darleen anijue

Tue, 9 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Nasra AbdallahMore by this Author Ishaq Mtoro ambaye ni mume wa msanii Queen Darleen amesema mke wake mkubwa ana mchango mkubwa katika maisha yake jambo lililosababisha hadi Queen Darleen kumjua.

Mtoro ameyasema hayo leo Jumanne Februari 9, 2021 katika mahojiano na kipindi cha mashamsham kuelekea siku ya wapendanao.

Kaka huyo amesema katika biashara ambazo anamiliki ikiwemo ile ya kuuza mabampa ya magari na kampuni inayojishughulisha na masuala y burudani , Sabra ana mchango mkubwa katika kuzifanya zisimame.

Alieleza zaidi kuwa mwanamke huyo ameishi naye miaka sita, na vitu vingi wamekuwa wakifanya naye pamoja hivyo hata hizo biashara anazomiliki kwa sasa ana mchango nazo.

“Mimi na Sabra tumeanziamaisha kutoka chini kwenda juu ambapo Queen alinikuta tayari anamiliki biashara mbalimbal,”amesema.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz