Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Irene Uwoya awasotesha waandishi nje ya ukumbi kwa saa tatu

81889 Pic+uwoya Irene Uwoya awasotesha waandishi nje ya ukumbi kwa saa tatu

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waandishi wa habari waliopewa mwaliko na msanii wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya kuhudhuria uzinduzi wa kipindi chake jana Jumamosi Oktoba 27, 2019 walizuiwa kuingia ukumbini hadi uzinduzi huo ulipomaliza saa nane usiku.

Licha ya kupewa kadi siku mbili kabla ya uzinduzi huo na kuwa na vitambulisho maalum, walizuiwa kuingia ukumbini kwa maelezo kuwa watazungumza na msanii huyo baada ya shughuli hiyo kumalizika.

Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne usiku na  kuhudhuriwa na wasanii na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Julai 17, 2019,  Uwoya aliwaomba radhi waandishi wa habari kutokana na kitendo chake cha kuwarushia fedha katika mkutano.

Aliomba radhi baada ya kumalizika kwa kikao kati yake ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) alikoitwa kutokana na kutumia mkutano huo kuwarushia fedha jambo  lililozua mjadala ikiwemo kuonyesha dharau kwa wana taaluma hao.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria uzinduzi huo jana ni Diamond Platnumz aliyeongozana na meneja wake, Babu Tale, Mwana FA, Elizabeth Michael maarufu Lulu,  Shilole, Esha Buheti, Steve Nyerere, Duma, Hemed Seleman, Yusufu Mlela, Happiness Magesa na  mtangazaji Zamaradi Mketema.

Pia Soma

Advertisement
Wakati wasanii hao wakiruhusiwa kuingia kwa kutumia mialiko yao, hali ilikuwa tofauti na waandishi wa habari kwani walilazimika kukaa nje ya ukumbi huo kwa zaidi ya saa tatu.

Mmoja wa walinzi waliokuwepo katika ukumbi huo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa amepewa maagizo kuwa wataishia nje baada ya kufanya mahojiano na Uwoya atakapowasili.

“Irene atakapofika nyie mtafanya naye mahojiano katika eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli  hii, ila kuingia ndani hamtaruhusiwa. Watakaoingia ni wale wenye mialiko,” amesema mlinzi huyo.

Wanahabari hao walipohoji mialiko na vitambulisho walivyopewa vilikuwa na umuhimu gani, walijibiwa kuwa hilo ndio agizo lililotolewa.

Hali ilikuwa tofauti alipowasili Uwoya saa 4:45 usiku kwani alijibu maswali yasiyohusiana na uzinduzi huo na kuahidi kuzungumza baada ya shughuli kumalizika.

Hali hiyo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuondoka huku wale waliobaki wakiruhusiwa kuingia ukumbini saa saba usiku baada ya uzinduzi jambo lililowafanya wakose picha za matukio yote muhimu.

SOMA ZAIDI:  Alichofanya Uwoya chalaaniwa kila kona

          :VIDEO: Irene Uwoya awaomba radhi waandishi wa habari, asema alitaka kuwatunza

         



Chanzo: mwananchi.co.tz