Mtandao maarufu wenye mabilioni ya wafuasi duniani kote, Instagram umeripotiwa kutokuwa hewani tangu jana Alhamisi saa 1:30 jioni huku watumiaji wake kutoka kila pande ya dunia wakilalamika kukumbana na adha hiyo.
Baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wenye watumiaji active bilioni 2.3 kwa mwezi, wameripoti kuwa wananshindwa kufungua mtandano huo kupitia application n ahata kupitia browsers.
Kupitia mtandao wa #Downdetector.com, imeelezwa kuwa mamilioni ya watumiaji wameripoti kushindwa kutumia Instagram tangu saa 2:30pm (AEST) sawa na saa saa 1:30 za jioni za Afrika Mashariki.
Watumiaji wakifungua mtandao huo unakuja ujumbe unaosomeka 'sorry, couldn't refresh feed' na 'something went wrong'.
Hii inakuja ikiwa ni wiki chache tangu mtandao huo kushindwa kupatikana na kusababisha adha kwa watumiaji 100,000 nchini Marekani na watumiaji 56,000 nchini Uingereza.
Updates:
Ijumaa, Mei 9, 2023, saa 5:30 asubuh, mtandao wa Instagram umeanza kupatikana kwa baadhi ya watumiaji wake.