Mkongwe kwenye gemu ya Bongo Fleva, Inspekta Haroun amemvaa Mwijaku kwa kumuambia anamshangaa anavyomsema yeye kwani hawatofautiani.
Ispekta amesema, yeye na Mwijaku wote wanalelewa hivyo hakuna ambaye anamcheka mwenzake na maneno mabaya aliyoyasema kuhusu yeye na Juma Nature, wameyachukulia kama challenge na sasa wameamua kurudi kufanya kazi.
“Mimi na Mwijaku hatuchekani, yeye analelewa na mimi pia nalelewa hivyo sioni tatizo. Mwijaku alitusema vibaya lakini kabla wahuni hawajamshughulikia, nimewatuliza na kuwaambia wamuache kwani hana nia mbaya na zaidi anatusaidia katika project yetu,” alisema Inspekta kwenye press ya wanahabari.
Inspekta na Juma Nature wana project yao ya kurudi mjini baada ya kupata mdhamini anayetajwa kwa jina la Gaza ambaye amedhamiria kuwarudisha wakongwe hao kwenye ramani ya muziki.