Wakongwe wanaofanya gemu kutokea pande za Temeke, Inspekta Haroun na Juma Nature, wamerudi kivingine baada ya kuandaa project yao mpya yenye nyimbo takriban sita.
Akizungumza na wanahabari juzikati, Inspekta alisema, kilichowapoteza kwenye gemu ilikuwa ni majukumu ya kimaisha lakini pia kushindwa kuwekeza mzigo wa maana kwenye muziki kutokana na majukumu hayo.
“Tunamshukuru Mungu kwa sasa amejitokeza bwana Gaza ambaye amejitolea kuweka mzigo ili tuweze kurudi mjini. Tumeshafanya Mzee wa Busara na kuna nyimbo nyingine kama sit hivi zitafuata.
“Tunaanza nah ii Mzee wa Busara sababu tunaona hili tatizo bado lipo mtaani, audio kafanya Mr T Touch na video kafanya Hanscana. Tunaachia audio na kisha video kisha mambo mengine yataendelea,” alisema Inspekta.