Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Imeisha hiyo! Hatimaye Kajala aipokea Range mpya aliyonunuliwa na Harmonize

Kajala Range 1 Kajala na Range mpya

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimnaye kwa mara kwanza, Msanii maarufu wa Bongo Movies, Kajala Masanja ameliposti gari jipya aina ya Range Rover alilonunuliwa na mpenzi wake, Harmonize ikiwa sehemu ya kumvuta mwanadada huyo kiurejeza katika himaya ya penzi la Mmakonde huyo.

Katika video iliyopistiwa na rafiki wa karibu wa Kajala aitwaye Cessy, anaonekana mdada huyo (yaani Cessy na si Kajala) akiwa mbele ya range hiyo huku akifurahia na kucheza, ameweka muziki na kuandika maneni mawili “Sa itakuwaje?”.

Video hiyo kutoka kwa Cessy ame-repost Kajala mwenyewe na kuongeza emoji za kucheka ikiashiria amefurahishwa na jambo hilo.

Hii inaashiria wazi kwamba huenda tayari Harmonize ameshamkabidhi Kajala gari lake hilo jipya lenye namba za usajili customized zinazosomeka jina lake yaani “KAJALA”.

Kajala na Harmonize waliingia kwenye uhusiano mwaka jana 2021, lakini uhusiano wao haukudumu sana baada ya video kusambaa zikidaiwa kuwa ni za Harmonize akimtongoza mtoto wa Kajala aitwaye paula ambaye kwa wakati huo alikuwa kwenye mahusiano na msanii kutoka WCB, Rayvanny jambo ambalo lilimtibua Kajala na kuamua kuvunja uhusiano wake na Harmo.

Mbali na kumnunulia Range mpya, Harmonize amekuwa akinunua zawadi kadha wa kadha na kuziposti mitandaoni akiambatanisha na jumbe za kuomba radhi kwa Kajala ili warudiane.

Wadakuzi wa masuala ya Udaku wanaelezwa kuwa tayari Harmonize na Kajala wameshamaliza tofauti zao hivyo wamerudisha penzi lao kama zamani na tutegemee kuwaona mastaa hawa kwa pamoja wakiwa hadharani muda wowote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live